Kocha Mkuu wa Coastal Union, Fikiri Elias amesema sababu kubwa ya kufanya vizuri na kikosi hicho ni ushirikiano mkubwa anaoupata kutoka kwa viongozi na umoja uliopo baina ya wachezaji wenyewe kwa wenyewe.

Kocha huyo tangu alipoongezwa kwenye benchi la ufundi kusaidiana na Joseph Lazaro, Februari, mwaka huu kikosi hicho kimecheza michezo sita bila ya kupoteza ambapo kati ya hiyo kimeshinda minne na sare mbili.

Kocha Fikiri amesema hakuna kitu kikubwa kilichobadilika ndani ya timu hiyo zaidi ya kutoa uhuru kwa kila mchezaji kucheza na kuonyesha uwezo baada ya wengi wao awali kutokuwa wakicheza.

“Malengo yetu kama timu ni kufanya vizuri katika michezo iliyobaki na ili kufanikisha hilo ni lazima tuwe wamoja,” amesema

Fikiri ameongeza licha ya kutojua hatima yake ndani ya timu hiyo baada ya msimu kuisha ila hilo halimuumizi kichwa kwani lengo la kwanza ni kuhakikisha kikosi hicho kinabaki Ligi Kuu kisha mambo mengine yatafuata.

Katika michezo Coastal chini ya Fikiri imefunga mabao sita ambayo ni wastani wa bao moja kwenye kila mchezo huku ikiruhusu mawili na kuiweka katika nafasi ya 10 na pointi 33 baada ya kucheza mechi 28.

Sadio Mane azigonganisha klabu za England
Tuna imani na kamati ya Majaliwa - Wananchi