Imeeleza kuwa Mshambuliaji na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane huenda akaondoka nchini Ujerumani mwishoni mwa msimu huu 2022/23, huku Klabu nne za England zikitajwa kumuwania ili kurudisha katika ligi ya chi hiyo.

Mane alijiunga na FC Bayern Munich Bayern akitokea Liverpool majira ya kiangazi mwaka jana kwa Pauni 27 milioni, lakini ameshindwa kuonyesha ubora Allianz Arena, akifunga mabao saba tu kwenye ligi, huku mara kadhaa akisumbuliwa na majeraha.

Hasira za Mane zilionyesha hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kuripotiwa alimpiga mchezaji mwenzake Leroy Sane baada ya Bayern Munich kuchapwa na Manchester City kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Na ripoti za Bayern zinadai kocha Thomas Tuchel hataki kuendelea na Mane.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, anahitaji Namba 9 asilia msimu ujao, lakini kuhusu Mane sio shida, tayari kuna klabu kadhaa za England zinapanga foleni kumsajili.

Chelsea ni miongoni mwa timu zinazomtaka Mane na mmiliki wa miamba hiyo ya Stamford Bridge, bilionea Todd Boehly hajawahi kuwa na shida kufungulia pochi usajili.

The Blues inahitaji kuboresha safu yao ya ushambuliaji baada ya msimu huu kufunga mabao 36 tu kwenye Ligi Kuu England.

Mane anaweza kwenda kumpa kocha Mauricio Pochettino maisha mazuri huko Chelsea kama usajili wake mpya.

Timu nyingine inayoweza kumchukua Mane ni Arsenal ambao watahitaji wachezaji wenye uwezo baada ya msimu huu kukosa taji la Ligi Kuu England kwa kukosa wachezaji wenye uzoefu wa kutosha kwenye kikosi chao.

Arsenal ilishika usukaní wa Ligi Kuu England kwa asilimia 93 ya msimu, lakiní sasa zikiwa zimebaki mechi zisizozidi tatu, tayari wameachia usukani kwa Man City.

Kocha Mikel Arteta ameona faida ya kuwa na wazoefu kama Jorginho na Leandro Trossard, hivyo atamhitaji Mane.

Wengine wanaoweza kumsajili Mane ni Newcastle United ambao watahitaji saini ya mkali huyo mwenye uzoefu mkubwa.

Kocha Eddie Howe anapambana kumaliza msimu ndani ya Top Four kwenye ligi ili kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya na kama hilo likitokea, basi watahitaji saini ya Mane.

Timu ya mwishoni Liverpool wanaoweza kumrudisha kikosini kwao staa huyo wa Senegal.

Mane alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu sana katika kikosi hicho cha Jurgen Klopp kilichobeba ubingwa wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Liverpool hawakutaka kumụuza mwaka jana, lakini ni Mane mwenyewe aliyelazimisha kuondoka.

Kwa sasa, Liverpool inahuduma ya mastaa kama Darwin Nunez, Mohamed Salah na Luis Diaz pamoja na Diogo Jota kwenye fowadi yake na kuna uwezekano mkubwa, Mane akarudi kwenye Ligi Kuu England msimu ujao.

Wakurugenzi CPB wapigwa msasa mafunzo utawala bora
Kocha Coastal Union afichua siri ya mafanikio