Licha ya kukabiliwa na changamoto ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United, Mshambuliaji Cristiano Ronaldo amefaniliwa kuitwa kwenye Timu ya Taifa ya Ureno itakayoshiriki Fainali za Kombe la Dunia baadae mwezi huu Novemba nchini Qatar.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 37, amekuwa na wakati mgumu wa kumshawishi Meneja wa Manchester United Erik ten Hag, huku akicheza michezo 16 msimu huu, akianzishwa kikosi cha kwanza mara 10 na kufunga mabao matatu.

“Wachezaji wote niliowata kwenye kikosi wana njaa ya kusaka mafanikio na kuipa kitu Ureno kwenye Fainali za Kombe la Dunia, hiyo imekua dhima kwangu kuwaita ili tukasaidiane kazi itakayotupeleka Qatar,” amesema Kocha Mkuu wa Kikosi cha Ureno Fernando Santos alipokua akitangaza kikosi.

Hata hivyo kwenye kikosi cha Ureno kilichotajwa na Kocha huyo, wachezaji wanaocheza Ligi Kuu ya England wapo 10 ambao ni Bruno Fernandes, Diogo Dalot (Manchester City), Joao Cancelo, Ruben Dias, Bernardo Silva, Joao Palhinha (Fulham), Jose Sa, Ruben Neves, Matheus Nunes (Wolves) na Ronaldo (Manchester United).

Timu ya Taifa ya Ureno imepangwa Kundi H, itaanza kupapatuana na Ghana Novemba 24 kabla ya kuikabili Uruguay Novemba 28 na itamaliza Hatua ya Makundi kwa kucheza dhidi ya Korea Kusini Desemba 02.

Kikosi kamili kilichotajwa tayari kwa Fainali za Kombe la Dunia 2022.

WALINDA LANGO: Diogo Costa (Porto), Rui Patricio (AS Roma) na Jose Sa (Wolverhampton Wanderers).

MABEKI: Joao Cancelo (Manchester City), Diogo Dalot (Manchester United), Ruben Dias (Manchester City), Raphael Guerreiro (Borussia Dortmund), Nuno Mendes (Paris St-Germain), Pepe (Porto), Danilo Pereira (Paris St-Germain) na Antonio Silva (Benfica).

VIUNGO: William Carvalho (Real Betis), Bruno Fernandes (Manchester United), Joao Mario (Benfica), Ruben Neves (Wolverhampton Wanderers), Matheus Nunes (Wolverhampton Wanderers), Otavio (Porto), Joao Palhinha (Fulham), Bernardo Silva (Manchester City) na Vitinha (Paris St-Germain).

WASHAMBULIAJI: Joao Felix (Atletico Madrid), Ricardo Horta (SC Braga), Rafael Leao (AC Milan), Goncalo Ramos (Benfica), Cristiano Ronaldo (Manchester United) na Andre Silva (RB Leipzig).

Kocha Walid Regragui ajilipua kwa Hakim Ziyec
Suarez, Cavani, Godin kuiongoza Uruguay safari ya QATAR