Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Youssoufa Moukoko ametajwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Ujerumani itakayoshiriki Fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza baadae mwaka huu nchini Qatar.

Mukoko ametimiza ndoto za kutajwa kwenye kikosi cha Mabingwa hao wa Dunia mwaka 2014, akitarajia kutimiza umri wa miaka 18 baada ya siku 10 zijazo.

Moukoko alifunga mabao mawili mwishoni mwa juma lililopita, wakati Dortmund ikiiadhibu Bochum kwa mabao 3-0, akithibitisha uwezo wake wa kuanzishwa kwenye kikosi cha kwanza cha BVB badala ya Anthony Modeste.

Shujaa wa Ujerumani aliyefunga bao la kuipa ubingwa wa Dunia nchi hiyo wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 Mario Gotze, naye ametajwa kwenye kikosi baada ya kuachwa 2018 kwenye Fainali zilizofanyika nchini Urusi.

Kikosi kamili cha Ujerumani ambacho kitakwenda kuwania Taji la Dunia nchini Qatar mwaka huu 2022, Walinda Lango ni Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre ter Stegen (FC Barcelona) na Kevin Trapp (Eintracht Frankfurt).

MABEKI: Armel Bella-Kotchap (Southampton), Matthias Ginter (Freiburg), Christian Gunter (Freiburg), Thilo Kehrer (West Ham), Lukas Klostermann (RB Leipzig), David Raum (RB Leipzig), Antonio Rudiger (Real Madrid), Nico Schlotterbeck (Borussia Dortmund) na Niklas Sule (Borussia Dortmund)

VIUNGO: Julian Brandt (Borussia Dortmund), Leon Goretzka (Bayern Munich), Mario Gotze (Eintracht Frankfurt), Ilkay Gundogan (Manchester City), Jonas Hofmann (Borussia Monchengladbach), Joshua Kimmich (Bayern Munich) na Jamal Musiala (Bayern Munich.

WASHAMBULIAJI: Karim Adeyemi (Borussia Dortmund), Niclas Fullkrug (Werder Bremen), Serge Gnabry (Bayern Munich), Kai Havertz (Chelsea), Youssoufa Moukoko (Borussia Dortmund), Thomas Muller (Bayern Munich) na Leroy Sane (Bayern Munich)

Wadau wateta na Wabunge mapendekezo sheria ya Habari
Ajali: Lori la Saruji lagonga magari Tegeta