Hatimaye Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Chelsea Hakim Ziyech amerejeshwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Morocco kitakachoelekea QATAR, miezi miwili baada ya kumaliza kifungo cha miezi 15.

Ziyech mwenye umri wa miaka 29 alilazimika kutangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Morocco mwezi Februari baada ya kuachwa kwenye kikosi kilichoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2021’ chini ya Kocha Vahid Halilhodzic, aliyesitishiwa ajira yake mwezi Agosti mwaka huu.

Hata hivyo Kocha Mkuu wa sasa Walid Regragui alijitwisha jukumu la kumuita mchezaji huyo na kumtumia katika michezo miwili ya kirafiki iliyochezwa mwezi Septemba dhidi ya Chile na Paraguay na sasa ameamua kumjumuisha katika kikosi kitakachokwenda QATAR.

Naye Beki wa klabu ya West Ham United Nayef Aguerd amatajwa kwenye kikosi kitakachokwenda QATAR Sambamba na nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain Achraf Hakimi na Noussair Mazraoui wa FC Bayern Munich.

Morocco imepangwa Kundi F na timu za mataifa ya Ubelgiji, Canada pamoja na Croatia.

Marocco inatarajia kucheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Georgia mjini Sharjah-Falme za Kiarabu (UAE) Novemba 17, kabla ya kuelekea QATAR tayari kwa mchezo wake wa kwanza dhidi ya Croatia utakaopigwa Novemba 23.

Kikosi kamili cha Morocco.

WALINDA LANGO: Yassine Bounou (Sevilla), Munir El Kajoui (Al Wehda) na Ahmed Reda Tagnaouti (Wydad Casablanca).

MEBEKI: Nayef Aguerd (West Ham United), Yahia Attiat Allah (Wydad Casablanca), Badr Benoun (Qatar SC), Achraf Dari (Stade Brest), Jawad El Yamiq (Real Valladolid), Achraf Hakimi (Paris Saint-Germain), Noussair Mazraoui (Bayern Munich) na Romain Saiss (Besiktas).

VIUNGO: Sofyan Amrabat (Fiorentina), Selim Amallah (Standard Liege), Bilal El Khannouss (Racing Genk), Yahya Jabrane (Wydad Casablanca), Azzedine Ounahi (Angers) na Abdelhamid Sabiri (Sampdoria).

WASHAMBULI: Zakaria Aboukhlal (Toulouse), Soufiane Boufal (Angers), Ilias Chair (Queens Park Rangers), Walid Cheddira (Bari), Youssef En-Nesyri (Sevilla), Abde Ezzalzouli (Osasuna), Abderrazak Hamdallah (Al Ittihad), Amine Harit (Olympique Marseille) na Hakim Ziyech (Chelsea).

Marekani ya kwanza kuwasili QATAR
Kocha Fernando Santos ambeba Ronaldo