Benchi la Ufundi la Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC limepata ufumbuzi wa beki wa kulia kwa kufanikisha usajili wa Israel Patrick Mwenda aliyetokewa KMC FC, ambaye atakuwa na jukumu la kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Shomari Kapombe.

Simba SC kwa kipindi kirefu ilikua haijapata mbadala sahihi Kapombe, licha ya msimu uliopita kumsajili David Kameta ‘Duchu’ lakini bado ilionekana hatoshi kuziba pengo la beki wa kulia.

Kaimu Afisa Habari wa Simba SC Ezekieli Kamwaga, amesema Gomes ameshusha pumzi yake baada ya kufanikiwa kupata mbadala sahihi wa Kapombe, jambo ambalo mwanzo lilikuwa likimnyima usingizi.

“Mashabiki wetu wengi awali walikuwa hawaamini katika usajili wetu wa vijana wenye umri mdogo tuliowapa nafasi msimu huu, ila kiukweli kwa benchi la ufundi sasa hivi linachekelea tu baada ya sajili hizi kuonyesha matunda hasa ukianza na safu ya ulinzi wa kulia, ambapo tumemuongeza Mwenda.

“Mwenda ana kiwango bora sana kiasi kwamba amemshawishi kocha, hadi hawazi tena kuhusu Kapombe hata akiumia kama ilivyokuwa mwanzo,” amesema Kamwaga.

Azam FC yageukia Ligi Kuu, yaipotezea Pyramids
Salam Jabir: Nikipewa nafasi Simba SC nitashukuru