Wakati Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Jumanne (Machi 28) kuikabili Uganda katika mchezo wa Kundi F, wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ Kocha Mkuu wa timu hiyo, Adel Amrouche, amesema katika mchezo uliopita wapinzani wao walijiandaa vizuri zaidi na waliwapa kazi kubwa sana ya kufanya ndani ya dakika 90.

Mchezo huo wa Kundi F, ulipigwa ljumaa (Machi 24) kwenye Uwanja wa Suez Canal Authority uliopo Jiji la Ismailia nchini Misri. Bao la ushindi liliwekwa kambani na Simon Msuva dakika ya 68.

Amrouche amefunguka: “Nawapongeza wapinzani wetu Uganda kwa kujipanga vizuri maana walitupa kazi kubwa sana ya kufanya ndani ya uwanja.”

“Hatma ya ushindi huu ilikuwa chini ya wachezaji wangu, kama kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi tulishafanya kazi yetu ipasavyo, kwa hiyo kila kitu kilikuwa chini ya wachezaji, wao ndyo walikuwa na maamuzi ya mwisho.”

“Naahidi nitafanya kila kitu kwa uwezo wangu kuhakikisha tunawapa furaha Watanzania na wale wote waliotupa sapoti yao kwenye mchezo huu.”

Stars iliyofikisha alama 04 katika msimamo wa Kundi F, itahitaji ushindi mwingine dhidi ya Uganda kesho Jumanne (Machi 28) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ili kuzisogelea fainali za AFCON 2023 zitakzopigwa Ivory Coast.

Al Hilal yaharibu dili la Ibenge Azam FC
Young Africans yatamba kuiangamiza TP Mazembe