Rais wa Shirikisho la soka nchini Rwanda(FERWAFA) Vincent Nzamwita amethibitisha kuwa shirikisho lake liko katika mazungumzo na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Kim Poulsen kwa lengo la kumpatia kibarua cha mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho hilo.

Amesema kuwa kocha huyo ni mwenye uzoefu mkubwa katika mipango ya maendeleo katika mpira wa miguu.

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF lilimfuta kazi Poulsen mwezi Februari 2014 kwa kile ambacho kilielezwa kuwa yalikuwa ni makubaliano baina ya pande mbili husika.

“Naweza kusema mazungumzo na Kim Poulsen yako katika hatua nzuri na kama mambo yatakwenda vizuri anaweza kusaini kuanza kazi hiyo mwisho wa mwezi huu na kuanza kazi mwezi Novemba. Mpaka kufikia sasa tumeshakubaliana mambo fulani” Nzamwita amekaririwa na vyombo vya habari nchini humo.

Kama atasiani mkataba huo, Poulsen atakuwa akisaidiwa na mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo (Amavubi) Jimmy Mulisa, na kazi yao kubwa itakuwa ni kusaka vipaji nchi nzima.

Kwa mujibu wa Nzamwita, Poulsen amechaguliwa na kuwashinda Michael Wise na mrundi Dominique Niyonzima kuziba nafasi ya mwingereza Lee Johnson ambaye zlijiuzulu kazi hiyo mwezi Aprili.

Kwa sasa Poulsen anaifundisha klabu ya Silkeborg IF ambayo inashiriki ligi kuu nchini Dernmark. Huko nyuma aliwahi kufundisha klabu ya Viborg FF.

Mbadala Wa Kaseja Azungumza
Super Sunday, Man Utd Vs Man City