Rais wa Iran, Hassan Rouhani anatarajiwa kuwasili mjini Tokyo leo kwa mazungozmzo na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe wakati kukiwa na mvutano kati ya Washington na Tehran kuhusiana na mkataba muhimu wa nyuklia na Iran.

Rouhani ambaye atakuwa kiongozi wa kwanza wa Iran kuitembelea Japan katika kipindi cha karibu miongo miwili iliyopita, atapokelewa na waziri mkuu Abe kabla ya wawili hao kufanya mazungumzo rasmi baadae leo.

Hapo awali Iran, ilisema mazungumzo kati ya Rouhani na Abe yatajikita katika mahusiano ya kiuchumi yanayoimarika kati ya mataifa hayo mawili na wala hayatogusia suala la tofauti kati ya Iran na Marekani.

Kwa upande wake Japan imesema inafanya juhudi za kidiplomasia kwa kushirikiana na mataifa yote ikiwemo Marekani na Iran ili kujaribu kupunguza mvutano na kurejesha amani katika eneo la Mashariki ya kati.

TCRA: Laini zisizosajiliwa kufungwa baada ya Desemba 31
Mnyika Katibu mkuu mpya Chadema