Mbunge wa Kibamba John Mnyika, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya jina lake kupendekezwa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, na kupitishwa na Baraza Kuu la chama.

Mnyika ametangazwa usiku wa kuamkia leo Disemba 20, 2019, ambapo amechukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Vicent Mashinji.

Aidha Baraza hilo pia limeridhia uteuzi wa Salum Mwalimu, kuendelea na nafasi yake ileile ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, ambapo pia baraza limemteua Singo Kigaila, kuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara na John Heche kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Ikumbukwe kuwa usiku wa kuamkia jana, wanachama wa Chadema walimchagua Freeman Mbowe kuongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano na Tundu Lissu ambaye awali alikuwa mwanasheria wao kuwa makamu mwenyekiti huku Said Mohamed makamu mwenyekiti Zanzibar.

Kwa mara ya kwanza Rais wa Iran Kuitembelea Japan
Vifo vya maralia vyapungua kwa asilimia 75 nchini