Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA, imeruhusu Mabasi yanayofanya safari za mikoani kuanza safari zake majira ya saa tisa usiku na kuagiza Wamiliki kufika ofisi za Mamlaka hiyo kuomba leseni na kuwasajili Madereva.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano – LATRA, Salum Pazzy na kusema usajili dhidi ya madereva hao utasaidia kupata taarifa zao.
Pazzy ambaye alikuwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania – TABOA, Priscus Joseph amesema LATRA inafanya kazi kwa kushirikisha na Wadau mbalimbali wakiwemo TABOA na wamekubaliana kuhusu muda wa kuanza safari hizo.
“Awali muda wa mabasi yote kuondoka ulikuwa saa 12 asubuhi na si zaidi ya hapo, lakini baadaye tuliruhusu ratiba zianze saa 11 asubuhi na sasa kwa pamoja tumekubaliana yaanze safari saa tisa usiku.”