Wachezaji wa tatu wa klabu inayoshika usukani wa ligi kuu wa soka nchini England, Leicester City wametajwa kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa msimu kupitia chama cha wachezaji wa kulipwa nchini humo PFA.

Wachezaji wa The Foxes waliotajwa kwenye orodha hiyo ni Jamie Vardy, N’Golo Kante pamoja na Riyad Mahrez ambapo wanaunga na kiungo wa West Ham Utd Dimitri Payet, mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane pamoja na kiungo wa Arsenal Mesut Ozil.

Wachezaji hao sita watakua wakiwania tuzo ya PFA itakayokua inashindaniwa kwa mara ya 43 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1973.

Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo itafanyika jijini London April 24.

Orodha nyingine iliyotolewa ni ile ya wachezaji wanaowani tuzo ya anaechikukia ambapo humo yupo mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane akichuana na mwenzake Dele Alli, mlinda mlango wa Stoke City Jack Butland, kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho pamoja na mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku sambamba na Ross Barkley.

Mwaka 2015 tuzo ya PFA ilichukuliwa na Eden Hazard wa klabu ya Chelsea huku tuzo ya mchezaji anaechipukia ikienda kwa Harry Kane.

Viporo Vya Young Africans, Azam FC Vyaliwa Kwa Shangwe
Picha: Waumini wamzawadia Mchungaji ‘Ndege Binafsi’