Waumini wa Kanisa la ‘Miracle Arena for All Nations’ lililoko Toronto nchini Canada na kuamua wamemzawadia mchungaji wao ambaye ni raia wa Ghana, ndege binafsi.

Ndege 1

Mchungaji Dk. Kofi Danso na mkewe Joanne Danso walianzisha kanisa hilo mwaka 2011. Februari mwaka huu katika sherehe za kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa (birthday), waumini wake walimzawadia usafiri huo.

Hata hivyo, Mchungaji huyo hakuonesha kushangazwa na zawadi hiyo na alieleza kuwa alikuwa amepewa maono na Mungu kuwa atapata ndege ya kutembelea mwaka huu, hivyo alivyokabidhiwa na waumini wake hakushtuka.

Alisema kuwa zawadi hiyo imemrahisishia usafiri kwani ataweza kufikia watu wengi zaidi duniani na kuhubiri injili.

“Kila kanisa linapaswa kumfanyia hivi Mchungaji wake kama linaweza. Kadri tunavyozidi kuwasaidia Wachungaji kufika bara moja na jijngine, ndivyo tunavyozidi kutimiza injili,” alisema Mchungaji Dk. Danso.

Mchungaji huyo alisisitiza kuwa usafiri huo kwake ni muhimu na sio anasa.

Leicester City Wachomoza Kivingine England
MARY MAJALIWA ATOA MSAADA KWA AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA