Rapa Lil Wayne amedaiwa kukiri kuwa aliwahi kujaribu kujiua kwa kujipiga risasi alipokuwa na umri wa miaka 12.

Awali, Weezy aliwahi kudai kuwa alijifyatulia risasi bahati mbaya alipokuwa na umri huo, lakini wakati huu ametoa maelezo zaidi na kukiri kuwa haikuwa bahati mbaya.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imewekwa pia na Billboard, Wayne amefunguka kwenye wimbo mmoja ambao uko ndani ya The Carter V ambayo haijatoka rasmi, kuwa kitendo cha kujifyatulia risasi iliyomjeruhi kifuani alikifanya makusudi akiwa anajaribu kujiua.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Lil Wayne anasema alifikia hatua hiyo baada ya mama yake kujaribu kumkataza asi-rap na aachane na muziki.

Ngoma ambayo imebeba maudhui hayo inadaiwa kuwa imechukua sample ya wimbo wa Sampha ya mwaka 2013 iitwayo ‘Indecision’. Weezy ametumia ngoma hiyo kwenye kionjo cha mwisho kwenye albam yake (autro).

Lil Wayne amewahi kuahidi kuwa atazungumzia kwenye albam yake hiyo matendo korofi aliyoyafanya alipokuwa mtoto.

“Wayne ameniambia kuwa anataka kuyaweka wazi mambo hayo ikiwa ni pamoja na tukio la kujipiga risasi,” Kiongozi mwandamizi wa Young Money, Mack Maine alisema.

Weezy alimaliza uhasama na mgogoro uliokuwa kati yake na Bosi wake Birdman kuhusu mkataba wa kutoa albam ya ‘The Carter V’.

Birdman aliomba radhi hadharani kuhusu mgogoro ulioibuka kati yao, hali ambayo ilitoa mwanga zaidi wa albam hiyo iliyosubiriwa kwa miaka saba.

Mara ya mwisho kwa Lil Wayne kuachia The Carter IV ilikuwa mwaka 2011.

Mama Muna afunguka mazito ya Muna, ''Muna ameniua''
Samia Suluhu atoa maagizo kwa wakuu wa mikoa