Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la ”Urithi Festival” amepongeza Wizara ya Maliasili na Utalii na watumishi wote wa wizara hiyo kwa kubuni na  kuanzisha tamasha la kuenzi Utalii hapa nchini ambapo matarajio ni kuongeza idadi kubwa ya watalii mpaka kufikia 2020.

Makamu wa Rais katika hotuba yake ametoa maagizo matatu likiwemo la kuwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wanatenga bajeti ya fedha kwa ajili ya kuadhimisha tamasha hili la Urithi Festival linalotarajiwa kufanyika kila mwaka Mwezi Septemba na kutaka Wizara husika kuandaa taratibu na sheria za kuadhimisha tamasha hili.

Suluhu amesema katika kuhakikisha malengo ya kuongeza idadi ya watalii yanakamilika serikali imefanya mambo mbalimbali kuhakikisha inatengeneza mazingira rafiki kwa watalii ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya barabara, reli, ujio wa ndege ambazo tayari zimeanza kufanya kazi na zitatumika kusafirisha watalii sehemu mbalimbali za Tanzania.

Aidha, Kuyaenzi haya yote Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa mafunzo ya bure kwa watanzania yatakayotolewa katika chuo cha utalii  ambapo watanzania watapata nafasi ya kufahamu namna bora ya utunzaji na kuenzi utamaduni na utalii unaopatikana nchini kwetu ikiwa ni pamoja na kutambua faida za utamaduni wa kitanzania na namna ya kuziendeleza.

Lengo kubwa la tamasha hili ni kuimarisha, kuendeleza na kudumisha utamaduni na mali kale za Watanzania.

 

 

Lil Wayne akiri kujipiga risasi kifuani alipokatazwa kuimba
Pambano la Mwaka: Canelo, Golovkin kumalizana leo