Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewataka maafisa elimu na ugani kutengeneza mkakati kwa kushirikiana na wazazi, ili kurahisisha upatikanaji wa chakula shuleni.
Chalamilameyasema hayo wakati akiwa katika kikao cha wadau wa elimu, kilichokuwa kikiwasilisha taarifa ya hali ya elimu na changamoto zilizopo Mkoani. Kagera.
Amesema, “ni muhimu sasa afisa elimu watengeneze mnyororo pamoja na maafisa ugani ili kuwasaidia wazazi sasa kuingia kwenye kilimo kinachoweza kuwasaidia kurahisisha kuchangia chakula shuleni.”
Agizo la Mkuu huyo wa Mkoa, linatokana na mpango wa chakula shuleni kutofikia malengo na hivyo kushindwa kuimarisha lishe za wanafunzi shuleni, hali inayopelekea wengi wao kutofanga vyema katika masomo.