Mwanasheria mkuu wa Chadema, Rais wa TLS, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Antipus Lissu, amesema atarudi yeye na dereva wake nchini Tanzania kwa mahojiano zaidi kwani wao ndo mashahidi wakuu.

Katika mahojiano yaliyofanyika Jijini Nairobi Kenya, Lissu amenukuliwa akisema “Dereva wangu ameniendesha miaka 15, nilitendewa tukio nikiwa nae na nitahojiwa nikiwa nae”.

Aidha Lissu amesema hali yake inaendelea vizuri na atakapopona atarejea nchini kwa ajili ya kuendeleza kile alichokiita mapambano dhidi ya serikali ya Mheshimiwa Magufuli.

Pia ameeleza kuwa matibabu bado yanaendelea ameshafanyiwa upasuaji mara 17 na kutolewa risasi 16 na bado risasi moja ipo mwilin mwake taratibu za kuitoa zinaendelea.

Katika hatua nyingine Lissu amewatoa hofu wanachama wa Chadema na Watanzania kwa ujumla kutokuwa na wasiwasi na baadhi ya viongozi wanakiokihama chama hicho na kujiunga CCM kwani suala hilo ni la kawaida na lilikuwepo tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

 

Simba kufanya makubwa Mapinduzi Cup
Video: Vigogo 180 kitanzini Takukuru, Makonda sasa kugharamia mkesha wa mwaka mpya