Mjumbe wa kamati kuu Chadema na Aliyekuwa Mgombea wa Urais Mh. Edward Lowassa amewataka baraza la vijana Chadema kujipanga kuimarisha chama kwa kuzunguka vijijini kwenye mashina na matawi ya chama hicho.

Leo akizungumza na vijana hao Mh. Lowassa amesema kuwa ili kushinda uchaguzi 2020 ni lazima chama kiimarishwe kwa kuhakikisha maeneo ya vijijini watu wanaimarika zaidi kutaka mabadiliko.

”Pumzi ya CCM ni kazi aliyoifanya Mwl Nyerere  miaka  ya nyuma ya kuzunguka mikoa 25 na mimi nilibahatika kuzunguka  mikoa 17, tulishinda kwa kishindo kwa kuwa chama kiliimarika sasa nataka Bavicha tuende vijijini CCM imepoteza mvuto”. alisema Lowassa.

Aidha Lowassa amewataka vijana hao kutoona aibu kwa kile wanachokifanya kwa kuwa vijana ni chachu ya mabadiliko katika nchi zote ulimwenguni.

Hata hivyo amewataka wanachama pamoja na vijana hao kumheshimu na kumlinda Mwenyekiti wa Chama chao kwani ndiye waliyemchagua awaongeze .

”Lazima tumheshimu Mwenyekiti Mbowe, tumlinde kama vile nyuki anavyomlinda malkia wake, tusimchukie kwani tulimchagua wenyewe”. aliongeza Lowassa.

Mrema kuwaombea msahama kwa Magufuli wafungwa wa Dawa za kulevya, Ujambazi kwa sharti hili
Bavicha Wajipanga kwa Mkakati Mwingine Kuhusu Mkutano wa CCM