Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ameendelea kusisizitiza kuwa yeye ndiye aliyeongoza katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na msemaji wake, Aboubakary Liongo, Lowassa amewataka wananchi kutokata tamaa na kudai kuwa ushindi wake uliporwa.

“Nawashukuru sana watanzania kwa kunipa kura nyingi kabisa. Tulishinda, dunia nzima inajua na wao wanajua, watanzania mmeonesha imani kubwa kwangu. Nawashukuru sana watanzania kwa uvumilivu wenu baada ya kushuhudia ushindi wenu ukiporwa,” taarifa hiyo inamkariri Lowassa akiwa katika mkutano wa kampeni jijini Arusha wiki hii. 

Lowassa alieleza kuwa hakutaka kutoa tamko lolote litakalosababisha machafuko kwa kuwa anawapenda watanzania wote.

Hata hivyo, Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25, Dkt. John Magufuli ndiye aliyeshinda kwa kupata kura 8,882,935 (asilimia 58.46) akifuatiwa na Edward Lowassa aliyepata kura 6,072,848 (asilimia 39.97), hivyo NEC ilimtangaza Dkt. Magufuli kuwa mshindi na baadae kuapishwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Azam FC Huenda Wakafunga Safari Ya Afrika Kusini 2016
CAF Waitega Dar es salaam Young Africans Ligi Ya Mabingwa