Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuwa anasoneshwa na namna hali ya maisha ya watanzania wengi inavyozidi kuwa ngumu.

Lowassa ameyasema hayo katika taarifa yake ya kuwatakia Waislamu wote mfungo mwema wa Ramadhani ikiwa ni siku mbili kabla ya waumini wa dini hiyo kuanza ibada hiyo ya mfungo Mtakatifu.

“Bei ya bidhaa mbalimbali zimezidi kupanda na zaidi kuadimika kwa sukari ambayo ni bidhaa muhimu sana hasa katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani,” alisema.

Aidha, Lowassa aliwaomba wafanyabiashara nchini kupunguza bei ya bidhaa muhimu zinazotumika hasa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili Waislamu waweze kutimiza ibada hiyo vizuri.

Lowassa amewaomba Waislamu kuliombea Taifa amani, mshikamano na utulivu katika sala zao.

Majaliwa:Mataifa yaliyoendelea yashirikiane na Serikali ya Tanzania kuwahudumia wakimbizi
Video: Diamond akabidhi msaada wa madawati 600 kwa Makonda