Katika hali iliyowashangaza wengi, muigizaji na mshindi wa Tuzo za Oscar, Lupita Nyong’o amedai kuwa yeye hajawahi kumiliki runinga na hana mpango huo.

Lupita alidai kuwa yeye hupata taarifa kwa njia nyingine lakini sio kupitia vituo mbalimbali vya runinga kama ilivyo kwa watu wengi katika dunia hii ya sayansi na teknolojia ya hadi 12D.

“Sina runinga nyumbani kwangu, napata habari kwa njia nyingine,” alisema Lupita Nyong’o na kuongeza kuwa yeye hupata pia habari kutoka kwa marafiki zake wa karibu ambao wanapata habari chapchap kama ilivyo app za habari na humueleza kwa muhtasari.

Inawezekana Lupita ni mtu wa aina yake na mastaa wenye tabia hii huwa wachache sana. Hata hivyo, tabia hii ya Lupita alikuwa nayo mmoja kati ya wanzilishi wa TV duniani, aliyepewa sifa ya kuwa ‘father of TV’, Vladimir K. Zworykin ambaye aliwapiga marufuku watoto wake kuangalia TV licha ya kuwa yeye ni mmoja kati ya waliochangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa runinga.

Claudio Ranieri Kustaafu Kazi Akiwa Na Leicester City
Ralph Krueger: Ronald Koeman Haondoki Southampton