Rais John Magufuli na Mkewe, Mama Janeth leo amekuwa Rais wa kwanza Tanzania kupiga simu ya surprise moja kwa moja kwenye kituo cha runinga kama mtazamaji wa kawaida akichangia yaliyokuwa yanajadiliwa kwenye kipindi.

Magufuli amezungumza moja kwa moja na watangazaji wa kipindi cha ‘360’ cha Clouds TV akiwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ikiwa ni pamoja na namna walivyochambua magazeti na mijdala mingine. Moja kati ya mijadala hiyo ilikuwa mjadala uliohusu ziara yake Benki Kuu.

Rais Magufuli pia aliisifu ‘Clouds Media Group’ kwa namna wanavyofanya kazi akiigusia tukio la ‘Malikia wa Nguvu’ lililolenga kutambua mchango wa wanawake nchini katika kuzitambua fursa na kuzifanyia kazi ipasavyo.

#Repost @cloudstv with @repostapp ・・・ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli leo asubuhi wamepiga simu moja kwa moja katika kipindi cha #Clouds360 na kuwapongeza Watangazaji hao kwa kazi nzuri wanayoifanya. Mh Rais alisema kuwa yeye ni shabiki namba moja wa kipindi hicho na anafurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na #CloudsMediaGroup kama zoezi zima la #MalkiaWaNguvu na mengine mengi. Wakimalizia kuonge na watangazaji wa #Clouds360 waliwataka nao wakati mwingine waje na wenzi wao katika kipindi sio kila mara waje wenyewe ?. Tunamshukuru Mh. Rais kwa kitendo chake hichi, hili linaonyesha kuwa tunaifanya kazi vizuri lakini pia ni faraja kwetu kwani tunaamini sisi ndio kituo cha kwanza Mh. Rais kufanya kitendo hiki. Mungu Ibariki Tanzania.

A photo posted by Clouds Fm (@cloudsfmtz) on

Makala: Bahasha yenye jina la 'Lady Jay Dee' ilisahaulika kwenye tuzo za 'Malkia wa Nguvu?
Magufuli amtumia Muhongo kuiondoa IPTL iliyozaa sakata la Escrow