Tarehe 12 Machi mwaka huu, kulifanyika tukio la kihistoria nchini la kutambua mchango wa wanawake kwa kuwatunuku tuzo zilizopewa jina la ‘Malkia wa Nguvu’. Tukio hilo lilifana na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Niwapongeze sana Clouds Media Group kwa ubunifu wa hali ya juu na namna wanavyoweza kuja na vitu vikubwa vinavyowainua na kubadili mtazamo wa jamii kwa muelekeo chanya. Ni msaada mkubwa wanaoutoa kwa kuwapa wanawake ‘ndoano’ badala ya ‘samaki’.

Wanawake wengi walitoa masomo yaliyosisimua akili na kuamsha ari ya utafutaji kwa wanawake wengi waliopo nchini. Kila aliyepewa tuzo alistahili kabisa kupewa tuzo husika na historia yake ilijieleza.

Pamoja na ‘ukamilifu’ na kufanikiwa kwake kwa kiwango kikubwa sana… sana. Kuna mtu mmoja ambaye huko mitaani anatajwa kuwa alistahili kuwa sehemu ya tuzo hizo kutokana na mchango wake pamoja na historia ya mafanikio yake akitokea chini kabisa, akilelewa na Clouds Media Group kabla ya kujitegemea na kuwa ‘bidhaa ya miraba minne’ (giant brand).

Huyu sio mwingine ni Judith Wambura maarufu kama ‘Lady Jay Dee’ ama Binti Komando.

Msanii huyu ni kielelezo cha mafanikio ya wasanii wengi sana hasa wa kike na amewainspire wasanii wengi ambao hivi sasa nao ni ‘mastaa’ kwenye game.

Jay Dee alianza maisha ya chini sana akilipwa mshahara wa shilingi 70,000 pekee kwa kazi yake ya kwanza kuajiriwa. Lakini leo kupitia muziki unaongelea kumpuni kubwa anayotembea nayo msanii huyo.

Binti Komando ana kila sifa ya kuwa ‘Malikia wa Nguvu’ kutokana na historia yake ya muziki ambayo imemfanya kuwa msanii wa Bongo Flava wa kike mkongwe ambaye hajaondoka kwenye ramani ya muziki na ana ushawishi mkubwa sana.

Kwa ufupi tu, Jide anafaa kuwa Malkia wa nguvu kwani ni moja kati ya wasanii wa kike wa kwanza kabisa kufanya R&B kwa lugha ya Kiswahili.

Miaka 14 iliyopita (2002) alikuwa msanii wa kwanza wa kike wa Bongo Flava kushinda tuzo ya ‘Msanii Bora wa Kike kutoka Tanzania’ na kutumbuiza kwenye tuzo kubwa Afrika, Tuzo za Kora.

Redd's Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred akikabidhi tuzo ya Msanii Bora wa Kike iliyokwenda kwa Bint Komando Lady Jay Dee.Anayeipokea tuzo hiyo ni aliyekuwa Mumewe, Gardener G. Habash

Redd’s Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred akikabidhi tuzo ya Msanii Bora wa Kike iliyokwenda kwa Bint Komando Lady Jay Dee.Anayeipokea tuzo hiyo ni aliyekuwa Mumewe, Gardener G. Habash

Aliwahi kubeba tuzo kadhaa… mwaka 2004 alishinda tuzo ya ‘Albam Bora ya R&B’ Kwenye Tuzo za Muziki Nchini. Mwaka uliofuata alishinda tuzo ya ‘Video ya Msanii Bora’ Kusini mwa Afrika. Hizo ni baadhi tu na mfululizo wake uliendelea kwenye tuzo za Kili na mwaka jana aliibuka na tuzo ya ‘Msanii wa Kike Anayependwa Zaidi’ kwenye Tuzo Za Watu.

Sio tu nyumbani Tanzania, Jide amekuwa akishinda tuzo za kimataifa hata katika siku za hivi karibuni.

Mfano, mwaka 2014, alishinda tuzo za AFRIMMA zilizotolewa Texas, Marekani, akishinda Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki.

Jay Dee na tuzo

Jay Dee ndiye msanii wa kike wa Bongo Fleva mwenye hits nyingi na Albam 7 nzito sokoni zilizofanya vizuri kila kipindi alichozitoa.

Anamiliki Bendi ya ‘Machozi’ pamoja na biashara kadhaa.

Albam za Jay Dee ni pamoja na Machozi (2000),Binti (2003),Moto (2005),Shukrani (2007), The Best of Lady Jaydee (2012), Nothing But The Truth (2013), Nimekusubiri (2015).

Kadhalika, Jide amekuwa na taswira chanya hata kwa makampuni yaliyompa nafasi ya kuwa ‘Balozi’.

Mwaka 2015, Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) ulimchagua kuwa Balozi wa Kampeni ya Kili Challenge.  Mwaka 2014, Hospitali ya Marie Stopes ilimchagua kuwa Balozi wa Kampeni ya Chagua Maisha inayopinga mimba za utotoni.

Kuonesha kuwa bado Jide ni Malkia wa Nguvu tena wa Moto, siku mbili zijazo, Lady Jay Dee anakuja na kitu kipya na ameshaonesha dalili kuwa kitakuwa kitu kikubwa sana ‘Lady Jay Dee Anaamka Tena’.

3 Days To Go Love From Vee Money ? #LadyJayDeeOfficialCountDown #NaamkaTena #TheReturnOfTheQueen @vanessamdee

A video posted by Lady JayDee (@jidejaydee) on

  “Amekuwa moja ya wasanii ambae anapeperusha bendera  kimataifa. na mwaka 2016 ni wa neema kwake,” Mohammed Dewji, Mtanzania ambaye hutajwa na Forbes kati ya matajiri wa Afrika anamuelezea.


Mengi nimeyaacha lakini kwa ufupi huu utakubaliana na mimi kuwa waandaaji wa ‘Malkia wa Nguvu’ walisahau bahasha yenye jina la Lady Jay Dee.

Note: Nafahamu kiundani mgogoro uliopo kati ya Lady Jay Dee na waandaaji wa tuzo hizo. Najaribu kutengeneza picha tu.

 

Wenger Aridhika Na Kiwango Cha Arsenal Dhidi Ya Barca
Magufuli na Mkewe wapiga simu ‘Live’ Clouds TV kama watazamaji wa kawaida