Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dokta John Magufuli amewataka wananchi kutochagua chama ambacho kina sera ya kuanzisha mfumo wa majimbo.

Akihutubia mkutano wa kampeni wilayani Urambo, Tabora Magufuli amesema kuwa utawala wa majimbo unaweza kuleta mafarakano , utengano wa kimaeneo na kufanya nchi ivurugike .

“Kuna chama hakina sera kinataka kutugawa kwa majimbo. Ukishatengeneza majimbo ya utawala, huo ndio mwanzo wa mfarakano kwa sababu kila jimbo litakuwa linajitegemea lenyewe, likiwa masikini, litakuwa masikini wa kutupwa,”amesema Magufuli.

“Sitaki nitoe mfano wa baadhi ya nchi ambazo ziliingia kwenye mtego wa majimbo na ukawa mfarakano wa maisha yote, haya ni mambo wanayofundishwa huko wanapotoka na lengo ni kuifanya nchi ivurugike” amesema Magufuli

Mgombea huyo leo  anaendelea na kampeni zake mkoa wa Tabora.

Lissu: Mchagueni yeyote Kigoma Mjini
Kinachoisumbua Namungo FC chaanikwa hadharani

Comments

comments