Mahakama Kuu mkoani Arusha leo Machi 3, 2017 inatarajia kutoa maamuzi ya maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema baada ya pingamizi la Jamhuri kuondolewa Mahakama ya rufaa February 27, 2017.

Viongozi wa Chadema, Freeman Mbowe, Edward Lowassa, Fredrick Sumaye pamoja na viongozi wengine wamewasili katika hiyo kusikiliza kesi ya Lema, ambapo hadi sasa pande zote zimeomba muda wa kuwasilisha hoja zao kwa maandishi na Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Salma Magimba amekubali na amewapa muda hadi saa saba na nusu mchana.

Man Utd Kuamua Hatma Ya Michael Carrick
Mahakama Kuu kutoa uamuzi kuhusu Lema leo