Wazazi Nchini wametakiwa kutowafanya watoto wao wa kike kuwa chanzo cha mapato, kwa kuwawekea kiwango kikubwa cha mahari pindi watakapokuwa wakihitaji kuolewa akidai kuwa suala hilo husababisha vikwazo kwa vijana wa kiume wanaotaka kuoa.
Hayo yamesemwa visiwani Zanzibar na mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Asha Suleiman Iddi katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya Qaswida.
Amewaasa wazazi wenzie kuacha tabia ya kuwafanya watoto wa kike kuwa chanzo cha mapato kwa kuwapangia mahari kubwa pindi wanapotaka kuolewa.
”Nawaasa wazazi wenzangu, msiwatumie vijana wenu wa kike kama chanzo cha mapato, mnawawekea mahari kubwa sana, mnasababisha vijana wakiume washindwe na waogope kujitokeza kuwaona,”amesema Mama Asha Suleiman
Awali akisoma risala, muandaaji wa mashidano hayo, Mwashaban Seif Ali amesema kuwa mashindano hayo yameanza kuonyesha muelekeo wa kukubalika ndani ya jamii kutokana na ongezeko kubwa la washiriki kutoka Madrasa 10 mwaka 2018 na kufikia hadi Madrasa 20 kwa Mwaka 2019.