Kufuatia uwepo wa mahudhurio hafifu ya wanafunzi katika shule za Sekondari za Ruhuwiko na Limbu, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas amewaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Viongozi ngazi ya kata na vijiji kuwakamata wazazi wote ambao watakuwa hawajawapeleka watoto shuleni hadi kufikia Januari 16, 2023.

Kanali Thomas, ametoa agizo hilo mara baada ya kusikitishwa na taarifa ya isiyoridhisha ya mahudhurio hasa kwa wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza, katika Wilaya shule hizo mbili za Wilaya ya Mbinga na Nyasa.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas.

Awali, akitoa taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi katika Wilaya hizo, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Aziza Mangosongo alisema mahudhurio ya wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza hayaridhishi.

Alisema, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Wanafunzi waliopangiwa kuripoti kidato cha kwanza ni 5,171 na kwamba hadi kufikia Januari 10, 2023 waliripoti wanafunzi 675 pekee, ambao ni sawa na asilimia 14.

Migogoro ndani ya ndoa yapata tiba kamilifu
Aliyeuwa watu 21 atengewa dola Mil. 10