Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amefika nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema ili kutoa pole na kuifariji familia.

Dkt. Mpango, amewasili nyumbani hapo kwa Marehemu Mrema eneo la salasala Jijini Dar es Salaam, akiongozana na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango hii leo Agosti 24, 2022 kwa poamoja ili pia kuwafariji ndugu , jamaa na marafiki kufuatia kifo cha kiongozi huyo kilichotokea Agosti 21, 2022 katika hospitali ya Muhimbili.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango alipofika kumfariji Bi. Doreen Kimbi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es Salaam.

Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amewaomba wanafamilia kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu na kwamba anatamabua wakati walionao lakini hakuna budi kushukuru kwa jambo hilo ambalo sote tutalipitia.

Amesema, Marehemu Mrema alikuwa ni kiongozi mkweli na mzalendo kwa Taifa, ambapo wakati wote alitetea maslahi ya nchi na ni wazi kuwa Taifa limepoteza kiongozi aliyetumikia vizuri nafasi zote alizowahi kuongoza wakati wa uhai wake.

Singida Big Stars yachimba mkwara mzito Ligi Kuu
Majirani wa Makamu wa Rais wagomea Sensa