Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa dili wanamuziki Mrisho Mpoto na Banana Zorro kuchagiza katika kampeni ya usafi wa jiji hilo kwa kuandaa wimbo maalum wa kuhamasisha.

Taarifa ya mpango huo ilianza kutolewa na Mrisho Mpoto kupitia Instagram kwa kupost picha inayowaonesha wakiwa na studio na Mkuu huyo wa Mkoa.

“Saa saba usiku, wakati wengine wamelala. sisi tupo macho studio, kujenga historia mpya ya Dar na Mh Mkuu wa Mkoa,” aliandika kwenye post yake yenye picha hiyo.

Akifafanua juu ya suala hilo baada ya kutafutwa na waandishi wa habari, Mrisho alieleza kuwa walikuwa wanaandaa wimbo maalum ambao utakuwa unatumika katika kampeni ya usafi katika jiji hilo.

“Ni wimbo ambao utakuwa unatumika katika kampeni za usafi wa mazingira katika Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Mrisho mpoto na kuongeza kuwa wimbo huo unatayarishwa na Allan Mapigo.

TFF, Bodi Ya Ligi Wapangua Tena Ratiba Ya VPL
Wabunge wa Chadema waanza kumuunga Mkono Magufuli