Malezi ya Viongozi wa Dini kwa Vijana yamekuwa na mchango katika kulinda amani ya Taifa, kupunguza matukio ya uhalifu na kuimarisha huduma mbalimbali za kijamii na kuwataka kuhimiza Watanzania kuzingatia mila na tamaduni ili kuimarisha misingi ya maadili.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hii leo Novemba 19, 2022 Jijini Dodoma wakati akitoa hotuba kwenye maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista Wasabato, Jimbo la Kati nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan akitoa Tuzo kwa Waasisi wa Injili wa Kanisa la Waadventista wa Sabato kwenye Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya kazi ya Utume na Huduma ya Jamii katika Kanisa la Waadventista wa wa Sabato yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma hii leo Novemba 19, 2022.

Amesema, “Nimefurahishwa na kwaya mbili hapa, wameimba maudhui ya kizalendo na wamejengwa kizalendo. Kwa hiyo niwashukuru sana kwa malezi hayo, ni jambo jema sana kwani bila kuwa na vijana waadilifu, basi magereza yetu yangekuwa yamejaa.”

Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, wakati wa Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya kazi ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania,  Jimbo la kati mwa Tanzania.

Hata hivyo, pia Rais Samia amelipongeza Kanisa hilo katika ushiriki wake wa kutoa huduma za kijamii kwenye sekta ya afya na elimu na kupongeza zaidi ya miaka 100 ya kuanzishwa kwa kanisa hilo.

Mpango atoa siku saba utatuzi changamoto ujenzi wa barabara
Zaidi ya kodi na tozo 230 zimefutwa: Mpango