Mulunesh Bujiga, mwanamke mwenye umri wa miaka 60 hutembelea katika eneo lililo karibu na mji wa Bishoftu ambalo ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, Boeing 737 Max 8.
Kwa mujibu wa CNN, mwanamke huyo ameeleza kuwa hutembelea eneo hilo na kufanya ibada akiwa na familia yake kila siku kuomboleza vifo vya ndugu zao ambao ni kati ya watu 157 waliokufa kwenye ajali ya ndege hiyo.
“Ninakuja katika eneo hili kila siku na familia yangu kuomba, maumivu na majonzi bado hayajaisha,” amesema mama huyo.
“Tutapumzika vipi katika hali hii ambayo watu wetu wengi wamepotea hapa? Damu zao na maumivu bado yako nasi,” ameongeza.
Mama Mulanesh anaishi Kilometa 2 kutoka eneo ambalo ndege hiyo ilianguka, eneo ambalo ni mwendo wa saa moja kwa gari kutoka jiji la Addis Ababa.
“Siku ile kile tulichokiona pale ni karatasi tu zilizotatuka, hakukuwa na kitu kinachofanana na binadamu pale,” ameongeza mama huyo.
Ameongeza kuwa amekuwa akihangaika kutafuta usingizi na kula lakini hadi sasa bado hajapata faraja ya kuondoa uchungu wa janga hilo.
Ndege hiyo ilianguka Machi 10 mwaka huu, dakika sita tangu iruke kutoka Ethiopia ikielekea jijini Nairobi nchini Kenya.