Mama wa nahodha na mshambuliaji wa mabingwa wa soka barani Ulaya timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amemjia juu mchezaji wa Ufaransa Dimitri Payet kufuatia rafu mbaya aliyoicheza wakati wa mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo.

Dolores Aveiro mama wa Ronaldo, anaamini Payet ambaye anaitumikia klabu ya West Ham Utd alifanya makusudi kumuumiza mwanae katika mchezo huo, hali ambayo ilizua tafrani miongoni mwa mashabini na wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno, pale ilipothibitika asingeweza kuendelea na mchezo.

Dolores aliandika katika mitandao ya kijamii: “Sikuwahi kumuona mwanangu akiwa katika hali kama ile (Kulia kwa uchungu).

“Soka ni mchezo wa kucheza mpira, na sio kumuumiza mpinzani wako, kama ilivyokua kwa mwanangu dhidi ya Payet.” Aliandika mama Ronaldo

Dolores Aveiro

Hata hivyo pamoja na maneno hayo makali, bado mama huyo alikiri kufurahishwa na ushindi wa bao moja kwa sifuri ambao uliiwezesha timu yake ya taifa kutwaa ubingwa wa barani Ulaya dhidi ya wenyeji Ufaransa.

Hatua hiyo pia ilidhihirisha kurejea kwa furaha ya Ronaldo ambaye alionekana mnyonge baada ya kutolewa nje ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na Ricardo Quaresma.

Everton Waitoa Jacho Chelsea Kwa Kalidou Koulibaly
Nadir Haroub: Iwe Isiwe Medeama Lazima Wakae Taifa