Kuelekea Mpambano wa mzunguuko wa nne wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22 kati ya Young Africans dhidi ya Azam FC, Mshambuliaji Prince Dube ametajwa kuwa tishio.

Young Africans watakua wenyeji wa Azam FC Jumamosi (Oktoba 30), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam saa moja jioni.

Msemaji wa Young Africans Haji Manara amemtaja Mshambuliaji Dube kuwa tishio katika mpambano huo ambao unatarajiwa kuwa na vuta nikuvute, kutokana na ubora wa vikosi vya pande zote mbili.

Akihojiwa na Wasafi FM mapema leo Jumatano (Oktoba 27) Manara alisema: “Mchezaji Pekee Pale Azam FC ninayemuogopa sana ni Prince Dube yule mtu ni hatari sana pamoja na Abubakar Sure Boy anaecheza soka Safi la kuvutia”

“Sisi kama Yanga Sc kazi Yetu kutoa ni Burudani tunaenda kutoa burudani safi katika mchezo ujao dhidi ya Azam FC”

“Tunaenda kusaka Pointi tatu kwa nidhamu kubwa sana lengo letu ni kupata point tatu dhidi ya Azam FC.”

Hata hivyo Abubakar Sure Boy ambaye ametajwa na Manara hatokuwa sehemu ya kikosi cha Azam FC, kutokana na adhabu ya utovu wa nidhamu inayomkabili katika kipindi hiki.

Young Africans inaelekea kwenye mchezo wa Jumamosi (Oktoba 30), huku ikishika nafasi pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 9, huku Azam FC ikiwa nafasi ya kumi ikiwa na alama 4.

Masau Bwire: Simba tulieni, msitetereke
Hitimana awatuliza Simba SC