Bondia kutoka nchini ufilipino, Manny Pacquiao, ametangaza kustaafu mchezo wa ngumi leo Jumatano (Septamba 29) akiwa na umri wa miaka 42.

Pacquiao alianza kucheza ngumi za kulipwa mwaka 1995 kwa kucheza pambano lake la kwanza Januari 22, 1995 na kushinda kwa pointi dhidi ya Edmund Enting, huku pambano lake la mwisho akilicheza mwezi uliopita akipoteza mbele ya Yordenis Ugas.

Katika kipande kidogo cha video chenye sekunde 20 alichoposti kwenye ukurasa wake wa facebook uliothibitishwa usikuwa wa jana jumanne, Pacquiao alisema: “Natangaza kustaafu kwangu, Kwaheri mchezo wa ngumi.”

Pacquiao ambaye ni seneta wa bunge la ufilipino, ameacha rekodi ya kuwa bondia pekee kushinda mataji ya dunia katika madaraja 8 ya uzito (Weight Division) aliyocheza, huku akishinda mataji kumi na mbili ya ubingwa wa dunia.

Hivi karibuni bondia huyo aliyecheza jumla ya mapambano 72, akishinda 68, sare mapambano mawili na kupoteza mapambano nane, alitangaza kugombea urais wa ufilipino katika uchaguzi ujao wa taifa la hilo.

Hivyo kukaa kwake pembeni katika mchezo wa ngumi ni katika harakati za kujikita zaidi kwenye ulingo wa siasa, kupambania nafasi ya kiti cha urais wa Ufilipino.

KMC FC wachimba mkwara ugenini
MSD kuanzisha kiwanda cha dawa za ngozi