Bondia machachari, Mfilipino, Manny Pacquiao anatarajia kupanda ulingoni tena nchini Marekani Jumamosi hii, MMG Grand Garden Arena, Las Vegas kupigana kwa mara ya tatu na bondia, Timothy Brandley.

Hili litakuwa pambano la tatu kati yao. Mwaka 2012, Brandley alimpiga Pacquiao lakini bondia huyo Mfilipino alilipa kisasi kwa kumpiga Brandley kwenye pambano lao la marudiano mwaka 2014.

Ikiwa ni miezi 11 tangu apoteze pambano dhidi ya Floyd Mayweather, Manny Pacquiao amesema kuwa pambano hilo la Jumamosi litakuwa la mwisho kwake. Amepanga kustaafu baada ya pambano hilo na kuingia rasmi kwenye siasa.

 

Sakata La Upangaji Wa Matokeo, Katibu Mkuu Wa TFF Kwenda Mahakamani
Serikali yatolea majibu taarifa za walimu kuanza kuvaa sare