Mlinda Lango wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Aishi Manula amesema kujituma na ushirikiano uliopo baina ya wachezaji wa klabu hiyo, ndiyo chachu ya timu yao kufanya vyema kwenye Michuano ya Mapinduzi itakayofikia tamati kesho Alhamis (Januari 13).

Simba SC ilitinga hatua ya Fainali ya Michuano hiyo kwa kuichapa Namungo FC mabao 2-0, huku Azam FC wakiichabanga Young Africans kwa changamto ya Mikwaju ya Penati 9-8.

Manula amesema anaamini umoja wao na kujituma wakati wote ndio chanzo cha matokeo mazuri, huku lango lao likiwa salama tangu Michuano hiyo ilipoanza Januari 02.

Amesema utofauti wa michuano iliyopita na ya mwaka huu kwa timu yao ni wachezaji wote kuwa pamoja kwa sababu ya kutokabiliwa na michuano ya kimataifa.

“Mwaka huu wachezaji wote tumeungana kwa pamoja ikilinganishwa na miaka iliyopita, miaka iliyopita ilibidi mwalimu agawe vikosi viwili wengine wajiandae kwa michezo ya kimataifa ambayo iliyokuwa ikitukabili kwa wakati huo,” amesema.

Katika hatua nyingine Manula amezungumzia mchezo wa fainali Aishi kwa kusema, utakuwa ni mchezo wenye maandalizi kwa timu zote mbili.

Amesema Azam FC ni timu kubwa na ina uzoefu wa michuano hiyo na Simba pia ni wazoefu hivyo timu zote zitafanya maandalizi ili kuhakikisha kila mmoja anapata anachohitaji kwenye mchezo wa kesho Alhamis (Januari 13).

Kocha wa makipa Young Africans afunguka
Ahmed Ally: Simba SC inatumia mfumo wake