Wakati Mashabiki na Wanachama wa Young Africans wakiendelea kujiuliza kwa nini mabadiliko ya Walinda Lango yalifanywa na Kocha Msaidizi Cedric Kaze, Kocha wa Mapika wa klabu hiyo Razak Siwa amejitokeza hadharani na kumkingia kifua Mlinda Lango Eric Johora.

Johora alipewa jukumu maalum la kudaka Mikwaju ya Penati kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC, akichukua nafasi ya Aboutwalib Mshery dakika za lala salama.

Kocha Siwa amesema: “Wakati mwingine mchezaji huingiwa na hofu ila si kwamba kocha alijifanyia maamuzi mwenyewe ya kumpanga Johora ni jambo ambalo tulikubaliana wote na wachezaji walilifanyia mazoezi kwa siku tatu.

“Hivyo Johora alijua kabisa kuwa ikifika penalti yeye analazimika kukaa golini kwani ndiye alifanya vizuri zaidi mazoezini nadhani alipatwa na presha ndio maana hakuonyesha uwezo.

“Kama makocha hatuwezi kukwepa lawama na Yanga ya sasa inahitaji matokeo mazuri na sio wachezaji wa kujaribu mechi zenye ushindani na kuhitaji ushindi.”

Mchezo huo wa Nusu Fainali ulimalizika kwa Young Africans kufungwa Mikwaju ya Penati 9-8 na kuipa tiketi Azam FC kucheza Fainali dhidi ya Simba SC iliyoitoa Namungo FC kwa mabao 2-0.

Tanzanite yatangulia Zanzibar
Manula afichua kilichoifikisha Simba SC fainali