Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ imewasili Unguja-Zanzibar kwa ajili ya Kambi ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ethiopia.

Tanzanite itacheza dhidi ya Ethiopia Januari 23 Visiwani humo, kabla ya kusafiri hadi Adis Ababa kwa mchezo wa mkondo wa pili.

Baada ya kuwasili mjini Unguja-Zanzibar wachezaji wa Tanzanite wameonekana kuwa tayari kwa mchezo huo, licha ya kukabiliwa na siku kadhaa za maandalizi ya kuikabili Ethiopia.

Timu hiyo ilisonga mbele kwenye harakati za kusaka tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia chini ya umri wa miaka 20, kwa kuifunga Burundi.

Fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20, zitachezwa Indonesia mwaka 2023 huku Ukraine akiwa Bingwa mtetezi.

Azam FC yatamba kuibanjua Simba SC
Kocha wa makipa Young Africans afunguka