Mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao mashariki mwa DRC, huku wengi wao wakikabiliwa na njaa na mara nyingi wanalazimika “kupigania” mgao mdogo wa chakula unaosambazwa na NGOs au Serikali ya Kongo.

Maelfu ya makazi madogo ya muda yamekuwa yakiratibiwa katika maeneo ya jinari na barabara inayoelekea upande wa kaskazini kutoka Goma, huku kukiwepo na dalili ya janga kubwa la kibinadamu linalokumba eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wakimbizi wakisafirishwa na Malori ya UNHCR. Picha ya Petersman/ DW

Tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba 2022, makumi ya maelfu ya watu wamekuwa wakitafuta maeneo yenye usalama, wakikimbia kundi la waasi la M23 ambalo linakabiliana na mapigano kati yake na vikosi vya Serikali.

Licha ya juhudi za misaada, watu wote waliofurushwa makwao waliohojiwa na kulalamikia suala la njaa, na wengi wao walielezea kuwa wanalazimika kupigania ili wapate chakula huku maradhi ya Kipindupindu yakilipuka kutokana na ukosefu wa usafi kwa kushindwa kuzingatia kanuni za afya.

Mtoto wa Rais ahukumiwa miaka 12 jela
SMZ kumaliza ushughulikiaji hoja za muungano