Mahakama nchini Msumbiji imewahukumu wakuu wawili wa zamani wa ujasusi na mtoto wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Armando Ndambi Guebuza kifungo cha miaka 12 jela kutokana na kashfa kubwa ya ufisadi inayojulikana kama “deni lililofichwa”.

Mkuu wa zamani wa ujasusi na usalama wa serikali, Gregório Leão, na mkuu wa zamani wa ujasusi wa kiuchumi, António do Rosário, pamoja na Armando Guebuza, mtoto wa rais wa zamani Armando Guebuza walihukumiwa na mahakama maalum katika mji mkuu, Maputo.

Tukio la usikilizwaji wa kesi katika Mahakama ya Msumbiji. Picha ya Eurasia review.

Kesi hiyo, ambayo ilihusisha dola bilioni 2 za mikopo ya siri kutoka kwa benki za kigeni kwa makampuni ya serikali ya Msumbiji, ilikuwa imeiingiza nchi katika mgogoro mkubwa wa kifedha na inahusiana na deni lililowekwa na serikalimwaka 2013 na 2014 bila idhini ya bunge ambayo ilisababisha IMF kuingilia kati na kusababisha kuporomoka kwa deni kuu mwaka 2016.

Hakimu Msimamizi, Efigénio Baptista amesema kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 102, kifungu kidogo cha 1 na 97, zote za Kanuni ya Adhabu ya mwaka 1986, mshtakiwa Armando Ndambi Guebuza anahukumiwa kifungo kimoja cha miaka 12 gerezani na faini ya meticais 102,000.”

Ndambi Guebuza, mtoto wa rais wa zamani wa Msumbiji Armando Guebuza, (aliyesimama) akiwa Jijini Maputo hapo jana Desemba 7, 2022 kwa ajili ya kusomewa hukumu dhidi yake katika kesi ya kashfa ya rushwa. Amefungwa jela miaka 12. Picha ya Alfredo Zuniga | AFP

Waziri wa zamani wa fedha, Manuel Chang, ambaye alitia saini mikopo hiyo, amezuiliwa nchini Afrika Kusini tangu 2018, akisubiri kurejeshwa kwa madai ya kutumia mfumo wa kifedha wa Marekani kutekeleza mpango huo wa ulaghai.

Makamu wa Rais Equinor atembelea eneo la ujenzi mradi LNG
Mapigano DRC yaumiza raia wasio na hatia