Sakata la mchezaji wa Jamuhuri ya Kongo Langa Lesse Bercy ambaye anadhaniwa hakuwa na umri chini ya miaka 17, limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa tetesi kuwa amefariki dunia.

Shirikisho la soka nchini (TFF) ambalo lilimkatia rufaa mchezaji huyo na kusababisha amri ya kufanyiwa vipimo kutolewa na CAF, limekiri kusikia taarifa hizo.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas ameiambia Dar24 kuwa mpaka sasa hakuna uhakika wa jambo hilo na amewataka wadau wa soka nchini kuwa na subira.

Amesema suala hilo limeibuka miongoni mwa wadau wa soka hapa nchini, na TFF haijafahamu kama kuna ukweli wowote kuhusu kifo cha mchezaji huyo ambaye hapo awali ilielezwa yupo katika mji ambao unakabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe huko Jamuhuri ya Kongo.

“Suala la kifo ni zito, mimi sijazungumzia suala la kifo, na ni uvumi tu ambao watu wanauvumisha na wala shirikisho hatujalizungumzia hilo jambo,” Alfred ameiambia  Dar24.com.

“Wenzetu waislamu wana usemi wao unaosena INNALLAH MAASWABIRIN, kwa hiyo ningetoa wito kwa wadau wa soka nchini wavute subra, tuone tutakua tumepangiwa kitu gani huko mbele. Tusiharakishe sana na wala tusikurupuke sana, wakati utasema (Time Will Tell),” aliongeza.

'Sh. bilioni 40 zimepelekwa Wizara ya Afya kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba' - Majaliwa
Azam FC Kusaka Vijana U-17 Kigoma J’mosi Hii