Rais mteule wa Marekani amesema atawaomba raia wa nchi hiyo kuvaa barakoa siku 100 za mwanzo za utawala wake ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha CCN Biden amesema kuwa itasaidia kupunguza maambukizi ya Corona kama kila Mmarekani atavaa barakoa.

Katika mahojiano aliyoyafanya na mwanahabari, Jake Tapper wa CNN, Biden amesema kuwa siku ya kwanza atakayo apishwa atawaomba wananchi kuvaa barakoa kwa siku 100 ili kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona.

“Na nadhani itaweza kusaidi kupunguza maambukizi kwa kiasi kikubwa sana, kama chanjo na barakoa zitaweza kupunguza maambukizi.” amesema Biden

Mpaka hivi sasa Marekani ina rekodi ya maambukizi ya corona milioni 14 huku vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ikiwa ni takriban 275,000.

TANAPA washindi tuzo ya dhahabu
Dar yapiga hatua matumizi njia za uzazi wa mpango

Comments

comments