Marekani imeiondola vikwazo vya kiuchumi nchi ya Sudan ikisema taifa hilo limeanza kuangazia maswala kuhusu kukabiliana na ugaidi pamoja na ukiukaji wa haki za kibinaadamu dhidi ya raia wanaoishi katika jimbo la Darfur.
Uamuzi wa Marekani unakuja ikiwa ni mwezi mmoja kupita baada ya rais Trump kuliondoa taifa hilo la Sudan katika orodha ya nchi ambazo watu wake hawaruhusiwai kuingia Marekani.
Hata hivyo uamuzi huo unaacha vikwazo vingine kuendelea kwa sasa ikiwemo vile dhidi ya watu binafsi walio na agizo la kukamatwa kufuatia unyanyasaji uliofanyika katika eneo la Darfur.
-
Mke wa Mugabe ashtukia mpango wa kumpindua Mumewe
-
Mpinzani wa Kagame afikishwa mahakamani Rwanda
-
Video: Lema, Marsha watuma salamu kwa watu ‘Wasiojulikana’
Sudan ndio taifa la pekee ambalo liliondolewa katika orodha hiyo wakati Venezuela, Chad na Korea Kaskani zikiongezwa ktika orodha ya nchi ambazo watu wake hawarusiwi kuingia Marekani.
Sababu zinazopelekea Marekani kuweka vikwazo kwa raia wa baadhi ya nchi kuingia Marekani humo ni pamoja na usalama wa nchi zao kuwa duni na ukosefu wa ushirikiano.