Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara, mama yake pamoja dada yake wamefikishwa mahakamani mjini Kigali kwa mara ya kwanza wiki mbili baada ya kuzuiliwa na polisi kwa kosa la kuchochea uasi nchini humo, mashtaka ambayo wameyakanusha wakisema yana misingi ya kisiasa.

Diane Rwigara mwenye umri wa miaka 35 alizuiliwa kugombea kiti cha urais baada ya Tume ya uchaguzi ya Rwanda kusema kwamba alifanya ulaghai katika kutafuta saini za wafuasi wake ili kutimiza matakwa ya tume hiyo.

Zaidi ya mashtaka hayo Diane ameshtakiwa kughushi nyaraka huku Mamake Adeilne Rwigara akishtakiwa pia kosa la kugawa wananchi kwa misingi ya kikabila.

Tangu ulipoanza mchakato huo wa kutaka kuingia ikulu,Diane Rwigara amejitokeza kama mpinzani na mkosoaji mkuu wa chama tawala RPF.

Na baada ya kukataliwa kugomea urais alianzisha vugugugu alilotaja kuwa na lengo la kupinga uonevu na kupigania haki miongoni mwa wananchi.

Diane Rwigara akiwa mahakamani

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Jumatatu wiki ijayo kutokana na watuhumiwa kutopata muda wa kutosha kuwasiliana na mawakili wao.

 

 

Fanani awafungukia ma-DJ ‘wanaompromoti shetani’
Mahakama yamfutia kesi Manji