Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa kama watu wasiojulikana wakiachwa waendelee kufanya masuala ya utekaji basi watu wataendelea kuishi kwa hofu ambayo imejengeka ndani ya mioyo yao.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa ni lazima watu hao washughulikiwe ili nchi iendelee kuwa na amani.

Kwa upande wake, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Awamu ya Nne, Lawrence Marsha amesema kuwa watanzania hawajalelewa katika maadili ya itikadi za vyama wala dini, hivyo kinachotakiwa ni kuitunza amani iliyopo.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wamekuwa wakilalamika kutishiwa na watu hao wasiojulikana hivyo wameliomba jeshi la polisi kuwasaka watu hao.

Mahakama yamfutia kesi Manji
Syria yajisogeza fainali za kombe la dunia 2018