Serikali ya Kenya imetangaza kupunguza matumizi katika baadhi ya taasisi za serikali ili kupata fedha kwa ajili ya kugharamia uchaguzi wa marudio wa Urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 17
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Henry Rotich, ambapo amesema kuwa tume mbalimbali pamoja na County zote 47 zitaathirika na uamuzi huo wa kubana matumizi.
Aidha, Rotich amesema kuwa tayari wametangaza kupiga marufuku safari za nje kwa baadhi ya viongozi wa serikali bila ya kibali maalum kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta.
Hata hivyo, uchaguzi huo wa marudio unatarajia kuligharimu taifa hilo la Afrika Mashariki Dola za Kimarekani milioni 150, na kwamba serikali haitarajii kukopa fedha nje kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi huo.