Mwenyekiti Mtendaji Fastjet Tanzania, Lawrence Masha amesema kuwa ni kweli shirika hilo lilikuwa na madeni lakini Mamlaka zingeshirikiana naye angehakikisha fedha hizo zinalipwa
Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani nchini anayemiliki asilimia 68 za hisa kwenye shirika hilo amesema kuwa Fastjet PLC ilianza kukusanya fedha na wameshakusanya Dola za Kimarekani Milioni 35
“Fastjet imelipa baadhi ya madeni yake, mengine yanalipwa na Fastjet PLC. Fedha nyingine tumekodi ndege na kulipia vibali, Mamlaka zinatakiwa kuniruhusu kufanya kazi ili nipate fedha za kulipa madeni mengine.”amesema Masha
Hata hivyo, Masha amesema kuwa ataendelea kuiheshimu Serikali na nchi kwa ujumla, kwasasa amesema yupo tayari kufanya kazi na TCAA, Wizara husika na Serikali yote kwa kipindi chake chote cha biashara