Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa anaeitumikia klabu ya Manchester United Anthony Martial hatausahau mchezo wa jana dhidi ya Albania baada ya kocha wake Didier Deschamps kumtoa nje baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Martial mwenye umri wa miaka 20 alianza mchezo wa jana  huku Paul Pogba na Antoine Griezmann wakiwa katika orodha ya wachezaji wa akiba.

Hata hivyo, Martial hakuwa katika kiwango kizuri kama ambavyo amezoeleka namna anavyowanyanyasa mabeki wa Ligi ya England.

Licha ya kutoonesha kiwango hicho pengine kutokana na uzoefu wake mdogo katika michuano hiyo, lakini mashabiki hawakuacha kumponda kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Angalia walichomfanyia huku kwenye Twitter.

Yasemavyo Magazeti Kuhusu Usajili Wa Barani Ulaya
Simon Msuva: Sina Shaka Na Hassan Kessy