Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutangaza matokeo rasmi ya nafasi ya urais na kuanza na majimbo matatu ya mkoa wa Mtwara ambapo mgombea urais wa CCM, Dkt. John Magufuli ameongoza.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, Magufuli ameongoza katika majimbo matatu  ya Makunduchi, Paje na Lulindi yaliyotangazwa rasmi na Tume.

Ushindani mkubwa umeendelea kuonekana kati ya wagombea wawili, Edward Lowassa (Chadema) na Dkt. John Magufuli (CCM).

Katika jimbo la Makunduchi, Dkt. Magufuli amepata kura 8,406 sawa na aslimia 81 ya kura zote huku Lowassa akipata kura 1,769 sawa na asilimia 17.09 ya kura zote zilizopigwa ambazo ni 10682.

Wagombea wengine wa nafasi za urais wamegawa asilimia takriban 2 ya kura zote zilizopigwa.

 

 

Maalim Seif Ajitoa, Aweka Takwimu Zake Hadharani
Ester Matiko Atangazwa Rasmi Kuwa Mbunge Wa Tarime Mjini