Kocha Msaidizi wa Mabingwa Wa Soka Tanzania Bara Simba SC Seleman Matola ametabiri mchezo dhidi ya Coastal Union utakuwa mgumu.

Simba SC kesho Jumapili (Julai 11), itakuwa mwenyeji wa Coastal Union kutoka Tanga, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar ea salaam.

Matola amesema ugumu wa mchezo wa kesho unatokana na hitaji la vikosi vyote viwili, ambapo Simba SC wanahitaji alama moja ili kutangaza Ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

Coastal Union inahitaji alama tatu ili kujiondoa kwenye janga la tinu zitakazoshuka daraja msimu huu 2020/21.

“Sisi tunahitaji alama moja ili tutangazwe rasmi mabingwa lakini Coastal wanahitaji pointi tatu ili wajinasue na janga la kushuka daraja na hili litaufanya mchezo wa kesho kuwa mgumu, tupo tayari kuwakabili.”

“Tutapumzisha baadhi ya wachezaji lakini kikosi hakitakuwa na mabadiliko makubwa,”

Simba SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 76 huku Coastal Union ikishika nafasi ya 17 ikiwa na alama 34 juu ya Mwadui FC iliyojihakikishia kucheza Ligi Daraja La Kwanza msimu ujao.

Azam FC yairarua Trans Camp
Wakurugenzi wote wa halmashauri za Unguja Nje